Mwanafunzi anatakiwa kuhudhuria vipindi vyote vya masomo ndani na nje ya darasa na kuandika kazi zote zinazotakiwa kwa muda mwafaka, hata masomo yanayotolewa siku za jumamosi.
Mwanafunzi akishaingia shuleni haruhusiwi kutoka nje ya shule kabla ya saa ya kutoka bila ruhusa ya uongozi wa shule.
Mwanafunzi anatakiwa kutumia lugha ya kiingereza katika mawasiliano shuleni.
Kila mwanafunzi anapaswa kuvaa sare rasmi ya shule.
Kila mwanafunzi anatakiwa kuishi na kuendana na malezi mema aliyofundishwa na mzazi/ mlezi au hapa shuleni kama vile; kusalimiana, kula kwa adabu, kuepuka wizi au udanganyifu na kutotumia lugha za matusi.
Mwanafunzi akiwa mgonjwa, mzazi/mlezi atapewa taarifa na uongozi wa shule.
Kila mwanafunzi anatakiwa kula chakula kinachopatikana shuleni.
Mwanafunzi haruhusiwi kuja na chakula shuleni au fedha au kinywaji atakula chakula kinachopatikana shuleni.
Mwanafunzi asipohudhuria shuleni kwa muda wa siku 90 bila taarifa, atakuwa amejifukuzisha shule.
Mwanafunzi akiharibu mali ya shule au ya mwanafunzi mwenzake kwa makusudi, mzazi/mlezi atawajibika kulipa.
Kuchelewa kwa aina yoyote wakati wa kufungua shule likizo fupi au ndefu ni kosa.
Kila mwanafunzi anatakiwa afikishe wastani wa 85% katika mitihani yake.
Mwanafunzi hawaruhusiwi kuvaa mavazi au kutumia vitu vya mwenzake.
Mwanafunzi hawaruhusiwi kulala wawili kitandani.
Mfumo wa malezi ni wa kikatoliki, hivyo kila mwanafunzi anatakiwa kufuata kanuni za malezi yanayotolewa ili ajijenge vizuri kitabia.
Mwanafunzi yeyote haruhusiwi kusuka nywele,kuvaa hereni, bangili, cheni(mkufu), kupaka rangi au ina kwenye kucha.
Mwanafunzi yeyote haruhusiwi kusoma tuition kwa mwalimu anayefundisha shule hii.
Wazazi / Walezi hawaruhusiwi kuonana na mwanafunzi wakati wa masomo isipokuwa kwa kibali kutoka kwa mwalimu Mkuu.
Mwanafunzi anapaswa kuwatii na kuwaheshimu viongozi wa shule, walimu viranja na watumishi wote wa shule.